Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."

5/22/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."

Duration:00:00:42

Ask host to enable sharing for playback control

22 MEI 2026

5/22/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililohudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Amon Manyama, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania. Rashid Malekela wa Idhaa hii alituwakilisha na amezungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno kama neno "PEKEPEKE."Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa UNCERF umetoa dola milioni 60 kusaidia muitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC. Tayari vifaa tiba vimewasilishwa nchini humo na sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine wanaendelea na usaidizi ikiwemo kuweka vituo vya kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi na kuhakikisha utunzaji salama wa wagonjwa..Mwakilishi wa mpya wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Togolani Mavura amewasilisha rasmi nyaraka zake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jijini New York Marekani na kueleza yale aliyokuja nayo.shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema fedha zinazotumwa nyumbani na watu waishio ughaibuni au diaspora sasa zimezidi kiwango cha fedha za misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. IOM imeeleza pia namna diaspora walivyo na msaada mkubwa wakati wa majanga kwa kutuma fedha haraka, huduma na usaidizi kupitia mitandao ya kuaminika katika nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Haiti, Ufilipino na Ukraine.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”

5/21/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”

Duration:00:01:06

Ask host to enable sharing for playback control

21 MEI 2026

5/21/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi.Hadi sasa Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewasili Bunia, mashariki mwa DRC, ndani ya siku nne kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya maabara, PPE na mahema ya kuhudumia wagonjwa. Wakati huo huo MONUSCO inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu njia za kujikinga, huku WHO ikisema zaidi ya watu 600 wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa tangu mlipuko huo kuanza.Tukisalia na Ebola, Ili vifaa vya Ebola vifike kwa wakati, wako mashujaa nyuma ya pazia wanaohakikisha kila mzigo unasafiri salama. Miongoni mwao ni Milton Oloo, mwenye miaka 30 ya uzoefu wa kupakia mizigo JKIA nchini Kenya, ambaye sasa yuko mstari wa mbele kusaidia safari za ndege za Umoja wa Mataifa, UNHAS. “Tunachokifanya hapa leo ni kuhakikisha kwamba mizigo inayoelekea Congo DRC imepangwa vizuri na kupakiwa ipasavyo ili isiharibike. Pia naona fahari na Maisha ya watu yanayookolewa nafurahi”.Na jukwaa la 13 la miji dunini WUF13 linaelekea ukingoni Baku Azerbaijan likijadili changamoto ya makazi duniani, Rehema Kishoa kutoka Tanzania Mkurugenzi Msaidizi wa Uzingatiaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi anasema wao wamechukua hatua kukabili changamoto hiyo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

20 MEI 2026

5/20/2026
Hii leo kwenye Jarida la Habari tuna Muhtasari na Mada kwa Kina.MUHTASARIOngezeko la idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRCUmuhimu wa kushirikisha jamii kwenye udhibiti wa Ebola Mpango wa Tanzania wa kukabiliana na makazi duniMADA KWA KINAInaangazia uchambuzi wa ripoti ya uanishaji wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania ambapo tumezungumza na Afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Hali iko vipi ? na nini kinafanyika kusaidia waliokumbwa na uhaba wa chakula.Msomaji wako leo ni Rashid Malekela

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

19 MEI 2026

5/19/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waaandishi wa habari kuwa “Kuna zaidi ya washukiwa 500 na vifo 130 vinavyohisiwa kutokana na ugonjwa wa Ebola, na maabara zimethibitisha watu 30 wanaugua ugonjwa huo.” Mbali ya DRC, wagonjwa wawili wamegundulika huko Kampala Uganda na mwingine raia wa Marekani ambaye amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi, wakati huu ambapo WHO bado inakumbwa na sintofahamu kuhusu chanzo cha mlipuko wa sasa wa Ebola DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD, limetoa ripoti ukionesha uchumi wa dunia unakabiliwa na mtihani mpya kutokana na mishtuko ya biashara, chakula na fedha inayosambaa kimataifa. Ripoti hiyo inaonya kuwa licha ya kuanza kwa mwaka kwa matumaini mazuri, hali ya kijiografia, vita na changamoto za masoko sasa zinatishia ukuaji wa uchumi duniani. UNCTAD inaeleza kuwa nchi zinazoendelea ndizo zilizo hatarini zaidi, zikikabiliwa na mtikisiko wa mitaji, mzigo wa madeni na hofu ya uhaba wa chakula. Shirika hilo linashauri mataifa kuchukua hatua za kuimarisha sera za uchumi, biashara na uwekezaji ili kujikinga na madhara ya mishtuko hiyo.Na panya wanazua balaa huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Wananchi wanasema kuwa panya wanaingia kwenye mahema kila siku, wanachafua akiba ya chakula, na kushambulia watoto wadogo nyakati za usiku. Ikumbukwe baada ya vita kusitishwa wananchi walirejea katika maeneo yao lakini kwakuwa nyumba zililipuliwa wengi wanaishi kwenye mahema huku mazingira yakiwa machafu na mifumo ya maji ikiwa haifanyi kazi na hayo ni mazingira mazuri kwa panya kuzaliana.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:10:29

Ask host to enable sharing for playback control

18 MEI 2026

5/18/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mlipuko wa Ebola nchini DRC na Uganda na ujumbe wa Profesa Mohamed Yakub Janabi Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika kuhusu hatua WHO inachukua kudhibiti ugonjwa huo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo..Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa 79 wa Baraza la Afya Duniani ulioanza leo mjini Geneva, Uswisi amesema changamoto za afya duniani hazijawahi kuwa kubwa kiasi hiki na hivyo akawakumbusha wahudhuriaji kwamba mkutano huu ni fursa muhimu kwa Mataifa Wanachama kuoanisha na kuharakisha juhudi za kukabiliana na changamoto za afya duniani..Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa nchi za Afrika kuwajumuisha wakimbizi, watu wasio na uraia, na wale walio katika hatari ya kukosa uraia katika mifumo ya kitaifa ya vitambulisho vya kidijitali. UNHCR imetoa ushauri huo katika mkutano wa ID4Africa uliofanyika mjini Abidjan, Côte d’Ivoire. Nchi za Kenya na Uganda ni miongoni mwa nchi zilizotumika kama mfano mzuri..Na kundi la watoto kutoka nchi mbalimbali lililotumia miezi 15 kuandaa muongozo waliouita ‘Tujumuisheni’ wakilenga kushughulikia upungufu katika ushiriki bora wa watoto kwenye uamuzi wa msuala mbalimbali kwa ngazi zote, wametoa wito kwa mashirika yanayofanya kazi na watoto na vijana kuutumia muongo wa viwango hivyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:11

Ask host to enable sharing for playback control

15 MEI 2026

5/15/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangazwa kwa mara nyingine kugundulika kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC katika jimbo la Ituri lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya 17 kwa mlipuko wa Ebola kutokea DRC tangu kugunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976. Wagonjwa 13 vimethibitishwa na taasisi ya utafiti wa tiba ya INRB mjini Kinshasa. Dkt. Tedros amesema tayari wametuma wataalamu, vifaa tiba na ameruhusu kutolewa kwa dola laki tano kusaidia kudhibiti mlipuko huo na kuwahudumia wagonjwa.Hali ya kibinadamu nchini Somalia inazidi kuwa mbaya kuliko ilivyotarajiwa hapo awali. Akuzungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi afisa mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia George Conway amesema “Hivi sasa Takriban watu milioni sita nchini Somalia amba ni sawa na mtu mmoja kati ya sita anakabiliwa na njaa ikimaanisha kuwa anaruka muda wa kula chakula, au anaenda siku kadhaa bila chakula cha kutosha. Watoto ndio wanaolipa gharama kubwa zaidi. Karibu watoto milioni mbili wana utapiamlo mkali, ikimaanisha kuwa wana utapiamlo mbaya na dhaifu kimwili, na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kuugua au kufa.”.Na leo ni siku ya Kimataifa ya Familia, Umoja wa Mataifa unasema maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia jinsi umaskini, ukosefu wa huduma muhimu na msaada mdogo wa malezi vinavyoathiri familia na kudhoofisha maendeleo bora ya watoto. Maadhimisho ya mwaka huu yanaweka mkazo maalum kwenye hatua jumuishi za ulinzi wa kijamii kama vile ruzuku za watoto, likizo za uzazi zenye malipo, huduma nafuu za malezi ya watoto na elimu ya awali kwa watoto wadogo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:10:40

Ask host to enable sharing for playback control

14 MEI 2026

5/14/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme iliyoko kaunti ya Samburu nchini Kenya, ambaye katika mahojiano na Flora Nducha ameelezea jinsi mila na desturi kwa wanawake na wasichana kutorithi chochote kwenye jamii yao zinavyoanza kuyoyoma. Pia tunamsikia kutoka Salome Gatakaa Araka wa FODDAJ ambalo ni Jukwaa la Maendeleo ya Wanawake, Demokrasia na Haki, nchini Kenya ni shirika la kiraia ambalo mwaka huu kwa mara nyingine lilishiriki mkutano huo wa CSW70. Baada ya kushriki vikao mmoja wa viongozi wa shirika hilo amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na ndio msingi wa mahojiano haya.Tunakuletea pia muhtasari wa habari zikiwemo za hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na Sudan, pamoja na masuala ya afya tukimulika yanaoendelea kuhusu virusi vya Hanta au Hantavirus.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Katibu Mkuu Antonio Guterres aaga Muungano wa Afrika na kutoa tathmni ya ushirikiano wa UN-AU

5/13/2026
Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.. Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye taarifa hii.

Duration:00:02:33

Ask host to enable sharing for playback control

13 MEI 2026

5/13/2026
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar.Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia..Mwenyeji wako ni Anold Kayandai, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

UNDPTanzania yajengea uwezo wasaidizi wa kisheria 126 kisiwani Pemba, ili kutatua migogoro kwa njia mbadala

5/13/2026
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. Rashid Malekela na taarifa zaidi.

Duration:00:02:48

Ask host to enable sharing for playback control

AfroKids International ni tumaini kwa wanawake wakimbizi barani Ulaya - Farina

5/13/2026
Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia.

Duration:00:03:19

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “Payapaya.’’

5/12/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya.’’

Duration:00:01:02

Ask host to enable sharing for playback control

12 MEI 2026

5/12/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Côte d'Ivoire ambako wakulima wameshuhudia kuimarika taratibu kwa uzalishaji wa kakao baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kusaidia wakulima nchini humo kurejesha ardhi katika ubora wake na kuongeza uzalishaji kupitia mbinu endelevu za kilimo mseto cha misitu, mazao na mifugo..Afrika imekuwa mstari wa mbele kushinikiza mfumo mpya wa kifedha unaozingatia usawa kwa nchi zinazoendelea. Na leo katika mkutano wa kuangazia mustakbali wa Afrika, Africa Forward huko Nairobi nchini Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezipongeza nchi za Afrika kwa kuongoza juhudi hizo za mageuzi ya mifumo ya fedha duniani. Kuhusu utajiri wa madini yanayopatikana Afrika kunufaisha nchi nyingine nje ya bara hilo Guterres amesema “Hakuna tena unyonyaji wala uporaji. Watu wa Afrika lazima wanufaike kwanza, na zaidi kutokana na rasilimali za Afrika.”.Taarifa mpya kuhusu virusi vya hanta ni kwamba hadi sasa wagonjwa walioripotiwa ni 11, na watu watatu wamefariki dunia. Kati ya wagonjwa hao, tisa wamethibitishwa kuwa na virusi vya Andes huku wawili wakihesabika kuwa wagonjwa wanaoshukiwa lilesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. WHO pia wameipongeza serikali ya Hispania kwa ushirikiano wake katika mchakato mzima wa kuwaondoa salama na kuwarejesha makwao abiria takriban 150 kutoka nchi 23 waliokuwa katika meli ya kitalii ya MV Hondius ambapo humo ndio mlipuko wa hanta ulipotokoea.ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hivi karibuni kuhusu Malengo ya Misitu Duniani, Global Forest Goals kwa mwaka 2026 ikieleza bayana kuwa misitu ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha uhakika wa chakula na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu duniani. Nchini Kenya mkazi mmoja ameeleza bayana jinsi wanavyonufaika na msitu asili wa Ngong ulioko takribani kilometa sita kutoka mji mkuu Nairobi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya’’Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Akili Mnemba au AI haiwezi kuchukua nafasi ya kuwa mama

5/11/2026
Je Akili mnemba AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake. Tuungane na Leah Mushi kusikia wamesema nini kuhusu AI.

Duration:00:03:03

Ask host to enable sharing for playback control

Siku ya Kinamama: Mama ni nguzo ya jamii na msingi wa haki za watoto

5/11/2026
Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa na Redio washirika wetu Domus.

Duration:00:02:42

Ask host to enable sharing for playback control

11 MEI 2026

5/11/2026
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres nchini Kenya, Akili Mnemba katika nafas iza ajira, na nafasi ya mama katika jamii ikiturejesha nchini Kenya kusikiliza simulizi za wamama.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika.Je Akili Mnemba, AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake.Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa na Redio washirika wetu Domus.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:11:21

Ask host to enable sharing for playback control

UN yawekeza dola milioni 340 Nairobi kuimarisha kitovu chake barani Afrika

5/11/2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika. Stella Vuzo kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi anafuatilia zira hiyo na hii hapa taarifa yake.

Duration:00:04:02

Ask host to enable sharing for playback control

08 MEI 2026

5/8/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:10:55